Ikiwa tunataka kuendelea kutumia uwezo wa simu katika ubora wake , kuichaji ni mojawapo ya njia maarufu zaidi kuitunza simu yako.Idadi kubwa ya watumiaji huwa hawafikirii juu ya kuchaji simu zao na kwa kawaida hufanya hivyo mara tu uharibifu unapokuwa tayari umeshatokea mfano simu haikai na chaji tena, simu imevimba betri na kadhalika..
Hizi hapa ni njia ambazo ni muhimu kuzifahamu ili kutunza simu yako
JINSI YA KUCHAJI SMARTPHONE YAKO VIZURI
Kuna makosa mengi unaweza kufanya unapochaji betri ya simu yako . Lakini wakati huu tutazingatia njia tatu za juu. Epuka makosa haya kadiri uwezavyo ili kuongeza muda wa matumizi ama uhai wa simu yako.
TUMIA CHAJI RASMI
Tumia chaja ya simu iliyokuja nayo kutoka kiwandani ,Miongoni mwa makosa ya watumiaji wengi wa simu za mkononi hawajali chaja zao hivyo humpelekea mtu kutumia chaja yoyote tu kuchaji simu yake.
Ikiwa umepoteza chaja yako ama kuharibika basi tembelea muuzaji wa vifaa vya simu Orijino kwa ajili ya kununua chaja inayoendana na simu yako.Tunaposema chaja ni Pamoja na waya wake kwa ujumla .
USIKUBALI SIMU IZIME CHAJI (0%)
Simu yako katu usikubali iwe inaisha kabisa chaji ndiyo unaichaji hii inaweza sababisha simu yako kuuwa betri ama kukataa kuwaka kabisa.
Na pia ukiichaji usichaji 100% sababu siyo salama zaidi kwa afya ya battery.watalaamu wanapendekeza 80% au 90% inatosha
USICHAJI USIKU KUCHA
Watu wengi huchaji simu zao wakati wa kulala kwa lengo kuwa akiamka iwe imejaa tayari. Hii siyo njia sahihi kuchaji simu yako kwa sababu madhala yake ni mengi .Simu inapokuwa imejaa chaji huwa inazuia chaji ya ziada kuingia ndani hivyo kupelekea simu yako kuchemka sana ambayo yaweza pelekea kuharibu mfumo wa kuchajia simu yako
Vile vile wakati unakuwa umelala unakuwa hujui hatari inayoweza kutokea kama umeme mfano kukatika ghafla ama kuja umeme mkubwa kupita kiasi hivyo kusabisha kuungua kwa simu yako na hata nyumba nzima.
ACHA KUTUMIA SIMU WAKATI UNACHAJI
Joto ni jambo linalouwa sana uwezo wa betri lako,Simu inapokuwa ina chaji huchemka na ukiongeza na matumizi wakati huo inachemka zaidi hivyo hupelekea betri kufa kabisa kwa muda mfupi ama kupungua uwezo wake wa kutunza chaji.
Kwa leo ni hayo tumekuandalia ,Endelea kufuatilia makala zetu ili uwezo kudumisha simu yako kwa ujumla....